Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MIGI ANASEMAJE KUHUSU NAFASI YA AZAM MBELE YA ESPERANCE?

MIGI ANASEMAJE KUHUSU NAFASI YA AZAM MBELE YA ESPERANCE?

Picha
Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’-kiungo Azam FC Kiungo wa Azam FC, Jean Mugiraneza ‘Migi’, amesema kuwa licha ya timu hiyo kukabiliwa na mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya Esperance, bado ina nafasi ya kusonga mbele kwa kuwatoa waarabu na kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho Afrika. Azam FC tayari imewasili nchini Tunisia tangu jana kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano utakaofanyika kesho Jumanne saa 3.00 kwa saa za Afrika Mashariki, wameingia wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-1 waliyoyapata awali jijini Dar es Salaam. Akizungumza na mtandao wa klabu  www.azamfc.co.tz  Migi amesema Azam FC ina wachezaji wengi wazoefu na wazuri jambo ambalo linampa matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo huo. “Nawajua Esperance, nimecheza nao mara nne nilipokuwa nacheza APR, mara zote nyumbani kwetu tulikuwa tunatoa nao sare au kushinda bao moja, lakini wamekuwa wakitufunga kwao, wanapocheza nyumbani wanapenda sana kumiliki mpira kwa kucheza...