Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Breaking News:Hamphrey Polepole Ateuliwa Kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma

Breaking News:Hamphrey Polepole Ateuliwa Kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Hamphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara. Bw. Hamphrey Polepole anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Musoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (Mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Uteuzi wa Bw. Hamphrey Polepole umeanza leo tarehe 18 Aprili, 2016 Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es Salaam 18 Aprili, 2016