Kutokwa na damu bila mpangilio Ukeni....
Tatizo hili huwasumbua wanawake wengi walio katika umri wa kuzaa na baadhi ya wanawake ambao tayari wameshafikia ukomo wa kuzaa. Kwa mwanamke aliyekwishafunga kupata hedhi kuendelea kupata damu ya hedhi au kutokwa na damu ukeni bila ya mpangilio siyo hali ya kawaida. Mwanamke anaanza kuvunja ungo kuanzia umri wa miaka 12 na hufikia ukomo kuanzia umri wa miaka 45. Kupatwa na damu ukeni chini ya umri wa miaka 40 kuna vyanzo vingi kama tutakavyoona. Chanzo cha tatizo Damu kutoka bila ya mpangilio kwa mwanamke ambaye hajakoma hedhi husababishwa na mabadiliko katika mfumo wa homoni endapo hazipo sawa ‘Hormonal Imbalance.’ Uwepo wa uvimbe katika kizazi na matumizi ya dawa za homoni mfano sindano au vipandikizi. Kuweka kitanzi katika kizazi pia huwafanya wanawake wengine wapate hali hii ya kutokwa na damu bila mpangilio. Mabadiliko ya mfumo wa homoni huweza pia kusababishwa na mshtuko wa mwili au hali ya mabadiliko ya mazingira. Kuharib...