Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Spika wa Bunge Job Ndugai Awaonya Wabunge Kuhusu Kujihusisha na Rushwa.......Awataka Wajiandae Kuupokea Muswada Unaozuia Wafanyabiashara Kuwa Wanasiasa

Spika wa Bunge Job Ndugai Awaonya Wabunge Kuhusu Kujihusisha na Rushwa.......Awataka Wajiandae Kuupokea Muswada Unaozuia Wafanyabiashara Kuwa Wanasiasa

Picha
Spika wa Bunge, Job Ndugai, ametaja sababu zinazochochea wabunge kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa, ni presha kutoka kwa wananchi inayotokana na kutakiwa kuchangia masuala mbalimbali katika majimbo yao. Spika huyo pia amewatangazia rasmi wabunge kuwa Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inatarajia kuwasilisha bungeni  muswada wa sheria utakaotenganisha uongozi na biashara. Aliyasema hayo wakati akizungumza katika uzinduzi wa Chama cha Wabunge wanaopambana na Rushwa (APNAC), mjini Dodoma. Aliwataka wabunge hao kujiepusha na vitendo vya rushwa licha ya kuwa na maslahi madogo. Pia aliwataka wajiandae na sheria hiyo kutokana na ukweli kuwa katika bunge hilo wabunge wengi pia ni wafanyabiashara.  Presha za rushwa  Alitaja sababu za wabunge wa Tanzania kujiingiza kwenye rushwa ni presha za wananchi wao kuwataka wachangie kila inapotokea msiba, sherehe, madawati, madarasa, barabara hadi ada. Alisema kutokana na kipato kidogo cha fedha, wabunge wengi hu...