Hassan Kessy Aweka Wazi Namba ya Jezi Anayoitaka Endapo Yanga Ama Azam Watamsajili....
BEKI wa kulia wa Simba, Hassan Kessy ameweka wazi namba ya jezi anayoitaka kwa timu atakayohamia kuwa ni 25 ambayo ataitumia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano mingine. Championi Jumatano linafahamu kwamba, Kessy anawaniwa na Yanga na Azam FC hivi sasa kwani amebakisha mwezi mmoja tu katika mkataba wake na Simba, hivyo yupo kuzungumza na klabu yoyote. Hata hivyo, Kessy ni kama yupo huru kabisa kwani Simba imemsimamisha kucheza mechi tano ambazo zitachezwa ndani ya mwezi mmoja kwa kosa la kumchezea rafu Edward Christopher wa Toto Africans na kupewa kadi nyekundu. Inafahamika kwamba, Yanga ndiyo ipo kwenye nafasi kubwa ya kumsajili Kessy kwani inataka acheze beki ya kulia huku beki wake Juma Abdul akipandishwa juu kucheza kama winga. Akizungumza na Championi Jumatano, Kessy alisema jezi namba 25 ndiyo yenye bahati kwake na siri kubwa kwake, hivyo timu itakayofikia makubaliano mazuri ya kumsainisha, basi ihakikishe inampatia jezi hiyo. Kessy alisem...