Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CAVALIERS WATINGA FAINALI YA NBA.

LEBRON AWEKA REKODI, CAVALIERS WATINGA FAINALI YA NBA.

Picha
Cleveland Cavaliers wamefanikiwa kutwaa ubingwa wao wa pili mfululizo kwa kanda ya Mashariki na sasa wanasubiri mshindi kati ya Golden State Warriors dhidi ya Oklahoma City Thunder ambao hata hivyo Thunder wanapewa nafasi kubwa kutokana na aina ya mchezo wanaoucheza sasa mpaka kufikia kuongoza 3-2. Kwa LeBron James, hii ni mara ya sita mfuululizo kutinga Fainali ya NBA. Anakuwa mchezaji wa 8 kufanya hivyo katika historia ya NBA. James alifunga pointi 33, Kevin Love alikuwa na pointi 20 na rebounds 12, na klabu ya Cavaliers ikatinga fainali yao ya pili mfululizo kwa kuichapa Toronto Raptors 113-87 katika mchezo wa sita wa fainali ya Mashariki iliyofanyika alfajiri ya Jumamosi. Cavaliers itakuwa inataka kumaliza ukame wa miaka 52 wa kutokutwaa ubingwa wa NBA, ambao ni muda mrefu zaidi kwa mji wowote wenye timu angalau tatu za kimichezo. Hakuna timu inayotoka mji wa Cleveland ambayo imewahi kushinda taji lolote tangu Browns blanked Baltimore 27-0 kushinda NFL michuano ya mwaka 1964. ...