Rais mstaafu Jakaya Kikwete ametaja mali alizochuma alipokuwa madarakani kwa miaka 10.
RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE. Kamishna wa Tume ya Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda ameiambia Nipashe katika mahojiano maalumu katikati ya wiki kuwa Kikwete ameshawasilisha tamko la mali zake tangu aondoke madarakani Novemba 5, mwaka jana. Jaji Kaganda alisema Kikwete aliwasilisha fomu inayoonyesha mali alizozipata wakati akiwa madarakani kati ya 2005-2015, na alizozipata kabla hajangia madarakani kwa Sekretarieti yake. Nipashe ilizungumza na Jaji Kaganda kujua kama Kikwete alishatoa tamko kama Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 na kanuni zake zinavyoelekeza, lakini pia kufahamu idadi ya mali anazomiliki Rais huyo mstaafu na thamani yake. Kaganda alisema ni kweli Kikwete aliorodhesha mali zake zote kwa tume lakini Jaji huyo alikataa katakata kumwonyesha mwandishi wa habari hizi tamko hilo. Jaji Kaganda alisema sheria inazuia kumwonyesha mtu mwingine tamko la mali la mtu mwingine hadi kuwe na sababu ya maana ya anayehitaji, na pia kuwe na ulazima wa ku...