Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mwakyembe: Bora Tufe Masikini Kuliko Kuwapigia Magoti Wazungu

Mwakyembe: Bora Tufe Masikini Kuliko Kuwapigia Magoti Wazungu

Picha
DK. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria, amesema kuwa Tanzania ni bora iendelee kutaabika na watanzania wafe wakiwa masikini kuliko kuendelea kunyanyaswa na mataifa ya ulaya. Mwakyembe ambaye hata hivyo hakuyataja mataifa hayo lakini moja kwa moja ilionekana kuyagusa baadhi ya mataifa ya Ulaya pamoja na Serikali ya Marekani iliyovunja uhusiano na Serikali ya Tanzania katika mambo yote yanayohusu miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na mfuko wa changamoto za millenia (MCC). Mwakyembe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa wizara ya katiba na sheria jijini hapa, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi kwa mkoa wa Mwanza. Mwakyembe ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya, amesema kuwa anashangazwa na baadhi ya watu wanaotaka kuliingiza taifa katika mambo mabaya yasiofaa na yalioko kinyume na maadili ya watanzania. Amesema mataifa hayo yamekuwa yakionekana kuilazimisha Tanzania kuingia katika mambo yasiyokubalika na watanzania wenyewe ikiwemo sua...