UKAWA Wadai Rais Magufuli Ndo Chanzo cha Sukari Kuadimika Nchini
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema tatizo la sukari nchini limetokana na uamuzi usio sahihi wa Rais Dk. John Magufuli, kwa kupiga marufuku uingizwaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi bila kufanya tathmini. Akizungumza jana na waandishi wa habari, Waziri Kivuli wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Anthony Komu, alisema agizo hilo lilitolewa kwa kukurupuka na ndilo lililosababisha sukari kuadimika. Komu ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Vijijini, alisema kama malengo ni kulinda viwanda vya ndani, basi lisifanyike kwa sukari pekee kwa sababu viwanda vipo vingi na bado bidhaa zinaingia kutoka nje nchi. Alisema kuna harufu ya upendeleo kutokana na Rais kuwa swahiba wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ambaye ni mmiliki wa mashamba ya Mtibwa, hivyo amefanya hivyo kwa kupewa ushauri mbaya huku nchi ikiingia kwenye upungufu mkubwa wa sukari. Alihoji kwa nini apige marufuku kwenye sukari tu wakati kuna viwanda vya nondo, saruji na vinginevyo na vinaleta bidhaa...