Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MWANTIKA

CITY INAVYOJIPANGA UPYA, MWANTIKA, KAVUMBAGU NI CHAGUO LA PHIRI, VIPI KUHUSU NONGA?

Picha
Na Baraka Mbolembole KOCHA Kinnah Phiri raia wa Malawi anawahitaji wachezaji wawili waliomaliza mikataba yao katika klabu ya Azam FC, mlinzi wa kati, David Mwantika na mshambulizi raia wa Burundi, Didier Kavumbagu. Mwantika ilibaki kidogo asajiliwe Mwadui FC katika usajili wa msimu uliopita lakini urejeo wa kocha Stewart Hall ukambakiza mlinzi huyo ‘aliyejengeka’ katika timu ya Azam kwa mwaka mmoja zaidi ambako amefanikiwa kucheza zaidi ya game 20 katika michuano yote. Kavumbagu amemaliza mkataba wake wa miaka miwili kwa mabingwa hao wa 2013/14 na hakuwa na msimu mzuri baada ya kufunga magoli matano tu katika ligi kuu huku mara nyingi akitumika kama mshambuliaji chaguo la tatu, la nne au la tano nyuma ya nahodha, John Bocco, Muivory Coast, Kipre Tchetche, Mkenya, Allan Wanga au Ame Ally ‘Zungu.’ “Kocha Phiri ameona mapungufu mengi katika timu, mfano katika beki ya kati, baada ya Juma Nyosso kufungiwa ikalazimika tumtumie Haruna Shamte kama beki wa kat...