CITY INAVYOJIPANGA UPYA, MWANTIKA, KAVUMBAGU NI CHAGUO LA PHIRI, VIPI KUHUSU NONGA?


Na Baraka Mbolembole

KOCHA Kinnah Phiri raia wa Malawi anawahitaji wachezaji wawili waliomaliza mikataba yao katika klabu ya Azam FC, mlinzi wa kati, David Mwantika na mshambulizi raia wa Burundi, Didier Kavumbagu.

Mwantika ilibaki kidogo asajiliwe Mwadui FC katika usajili wa msimu uliopita lakini urejeo wa kocha Stewart Hall ukambakiza mlinzi huyo ‘aliyejengeka’ katika timu ya Azam kwa mwaka mmoja zaidi ambako amefanikiwa kucheza zaidi ya game 20 katika michuano yote.

Kavumbagu amemaliza mkataba wake wa miaka miwili kwa mabingwa hao wa 2013/14 na hakuwa na msimu mzuri baada ya kufunga magoli matano tu katika ligi kuu huku mara nyingi akitumika kama mshambuliaji chaguo la tatu, la nne au la tano nyuma ya nahodha, John Bocco, Muivory Coast, Kipre Tchetche, Mkenya, Allan Wanga au Ame Ally ‘Zungu.’

“Kocha Phiri ameona mapungufu mengi katika timu, mfano katika beki ya kati, baada ya Juma Nyosso kufungiwa ikalazimika tumtumie Haruna Shamte kama beki wa kati.”

“Alicheza vizuri lakini mwalimu ameona kuna ulazima wa kumsajili mchezaji hasa wa nafasi hiyo na Mwantika anaweza kucheza vizuri na Tumba Sued.” anasema chanzo cha habari hii ambaye ni mtu wa ndani wa timu hiyo iliyotingisha sana msimu wa 2013/14 ambao ulikuwa ni wa kwanza kwa timu hiyo ya Mbeya katika ligi kuu.

Paul Nonga ni kati ya washambuliaji waliopata kutamba City na mshambulizi huyo aliyeomba kuachwa Yanga alionekana Mbeya wiki iliyopita.

“Siwezi kusema lolote kwa sasa kuhusu Nonga kwa kuwa ni mchezaji wa Yanga. Mshambuliaji ambaye tunamtazama kwa sasa ni Kavumbagu ambaye ni mchezaji huru. Pia mwalimu amevutiwa na uwezo wake.”

Kwa ukaribu zaidi, tafadhali unaweza ku-LIKE PAGE yangu BSports. Utapata Updates za michuano mbalimbali.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA