Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Sera Ya Rais Magufuli ya Kubana Matumizi Yawaliza Wafanyabiashara Dodoma

Sera Ya Rais Magufuli ya Kubana Matumizi Yawaliza Wafanyabiashara Dodoma

Picha
Sera ya Rais John Magufuli ya kubana matumizi serikalini imekuwa majanga kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma, huku wizara nazo zikionja cha moto.  Katika kipindi hiki cha kuanza kwa mkutano wa Bunge la Bajeti, wafanyabiashara mkoani hapa wamelalamikia biashara kudorora tofauti na kipindi kilichopita.  Biashara kubwa zinazofanywa wakati wa vikao vya Bunge ni vyumba vya kulala wageni, usafiri wa teksi, kumbi za mikutano na vyakula.  Mkutano wa bajeti uliopita, vyumba vya kulala wageni katika mji wa Dodoma vilikuwa vimejaa hata kabla ya kuanza mkutano wa Bunge, lakini hali hiyo imekuwa tofauti baada ya jana karibu nyumba zote za kulala wageni kuwa na nafasi nyingi huku nyingine zikiwa hazina wageni kabisa. Mkutano huo unaoanza leo kupitisha bajeti za wizara na Serikali Kuu, huwa na mjadala mkali na maofisa wa wizara kutoka vitengo mbalimbali husafiri kutoka Dar es Salaam na sehemu nyingine nchini kwa ajili ya kusaidia utoaji wa majibu na hoja zinazotoka kwa wabunge....