TOP 7 YA WACHEZAJI WALIOFANYA MAKUBWA KWENYE SOKA WAKIWA NA JEZI NAMBA 7 MGONGONI
Suala la wachezaji kuvaa jezi namba flani mgongoni mara nyingi huwa linaongozwa na imani, hii hapa ni list ya wachezaji saba ambao wamewahi kufanya mambo makubwa kwenye soka wakiwa wamevaa jezi namba 7 mgongoni. 7. Robert Pires Robert Pires alidumu kwenye kikosi cha Arsenal kwa miaka 6 pekee lakini ilitosha heshima kwenye klabu hiyo na kuwa miongoni mwa wachezaji wa kukumbukwa kwenye historia ya Arenal. Baada ya mafanikio makubwa kwenye michuano ya kombe la dunia na Euro mwaka 1998 na 2000 akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa, Pires alijiunga na The Gunners na kukiongoza kikosi hicho kutwaa kombe makombe matatu ya FA na mataji mawili ya Premier League. Kutokana na mchango wake kwenye kikosi cha Arsenal katika miaka 6 aliyoitumikia, alichaguliwa na mashabiki kama mchezaji wa sita mwenye mchango mkubwa kwenye timu. 6. Luis Figo Nahodha wa aina yake kuwahi kutokea kwenye timu ya taifa ya Ureno ambaye alikuwa akivaa jezi namba 7 na kupata mafanikio makubwa. Winga mwenye uwezo ...