RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN ATOA PONGEZO KWA SERIKALI JAMHURI YA WATU WA CHINA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu ukiongozwa na Katibu wake Bw.Luo Zhijon,(wa tatu kulia) mara ujumbe huo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na Ikulu.] 02/06/2016. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo sekta ya afya. Dk. Shein aliyasema hayo leo katika mazungumzo kati yake na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China katika Kamati ya Jimbo la Jiangsu Bwana Luo Zhijun akiwa amefuatana na ujumbe wake uliofika Ikulu mjini Zanzibar. Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alisema kuwa azma ya Jimbo la Jiangsu kuendeleza mashirikiano yake kwa kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo nchini ni hatua moja wapo ya kukuza uhusiano wa kidugu uliopo kati ya...