Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Taharuki imetanda nchini Uganda baada ya kiongozi wa upinzani Dr Kizza Besigye

Taharuki imetanda nchini Uganda baada ya kiongozi wa upinzani Dr Kizza Besigye, ''kujiapishwa kama rais'' siku moja tu kabla ya kuapishwa rasmi kwa rais Yoweri Museveni .

Picha
Besigye akamatwa kwa 'kujiapisha' Uganda Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa kizuizi cha polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''. Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya juu''. Video hiyo imesambazwa mno kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii. Rais Yoweri Museveni kuapishwa Alhamisi Besigye anahitimisha 'kuapishwa kwake'' kwa kuonya kuwa ''endapo kutafanyika sherehe nyengine hapo kesho, basi itakuwa ni kinyume cha sheria kwani kulingana naye Museveni hakushinda uchaguzi wowote''. Mgombea huyo wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha upinzani cha Forum for dem...