Nyota yazidi kungaa kwa Donald Trump USA
Mchakato wa kumpata mgombea wa urais katika vyama vya Republican na Democratic nchini Marekani unazidi kushika hatamu huku nyota njema ikizidi kuoneakana kwa Mgombea Donald Trump wa chama chama cha Republican. Hii ni baada ya ya Trump kushinda mchujo wa uteuzi katika uchaguzi wa chama cha Republican kwenye majimbo matano uliofanyika jumanne hii, majimbo amabayo ameshinda mchujo wa kuteua mgombea urais ni Connecticut, Delaware, Maryland, Pennsylvania na Rhode Island. Licha ya ushindi huo Donald Trump anakumbwa na upinzani mkubwa sana kutoka kwa baadhi ya wanaharakati ndani na nje ya Marekani, hii ni kutokana na sera zake zinazochukuliwa kama ni za kibaguzi, mojawapo ya sera zake ni ile ya kujenga ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico. Trump bado ameendelea kushikilia sera zake na aliwaambia wafuasi wake New York kwamba hatabadilisha sera zake iwapo atachaguliwa kuwa rais. "Sibadiliki, Mnafahamu kwamba nil...