KUELEKEA FAINALI YA UEFA, FAHAMU MAMBO 14 MUHIMU KATI YA SIMEONE NA ZIDANE
Na Mahmoud Rajab Kesho Mei 28 katika dimba la San Siro, kutakuwa na pambano kali la fainali ya UEFA pale Real Madrid watakapokuwa wakichuana na mahasimu wao wakubwa Atletico Madrid. Hii imekuwa ni fursa adhimu sana kwa makocha wa timu zote mbili yaani Zinedine Zidane na Diego Simeone kuoneshana umwamba kutokana na wote kuwa na historia ya kuvichezea vilabu hivyo. Kwa kufahamu umuhimu wa pambano hili, tumeamua kukuletea baadhi ya mambo muhimu ya kukumbukwa kati ya makocha hawa hawa kuelekea pambano hili; Diego Pablo Simeone (El Cholo) amewahi kuitumikia Atletico Madrid kama mchezaji katika vipindi viwili tofauti (1994-97 na 2003-05).Zinedine Zidane alijiunga na Real Madrid kama mchezaji katika dirisha kubwa la usajili la majira ya joto mwaka 2001 na kudumu kwa miaka mitano mpaka msimu wa mwaka 2005-06 alipoamua kustaafu soka.Zidane aliichezea Real almaarufu Blancos michezo 227, akifunga mabao 49 na kubeba makombe sita ,likiwemo la UEFA ambapo alifunga goli la kipekee baada ya kupig...