Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Afisa Uchaguzi Halmashauri Ya Serengeti Ahukumiwa Miaka Saba Jela.

Afisa Uchaguzi Halmashauri Ya Serengeti Ahukumiwa Miaka Saba Jela.

Picha
AFISA uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Bw.  Julius Bujabhi Makwasa amehukumiwa kifungo cha Miaka 7 jela baada ya kupatikana na hatia ya Makosa 34 yakiwepo ya Rushwa. Mnamo mwaka 2013 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mara ilimfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Serengeti Afisa uchaguzi wa Halmashauri hiyo Bwana Julius Bujabhi Makwasa na wenzake wawili wakishitakiwa kwa makosa thelathini na manne yakiwemo ya matumizi mabaya ya fedha za umma, kuisababishia hasara Halmashauri ya Serengeti, kusaidia kutenda kosa, kughushi na kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri wao. Washitakiwa wengine katika shauri hilo la uhujumu Uchumi E.C.C 130/2013 lililokuwa likisikilizwa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mheshimiwa Ismail Emanuel Ngaile,  walikuwa  Bi Scola Daudi Mosi ambaye ni mtunza kumbukumbu wa Halmashauri hiyo na Bwana Dickson Julius Makwasa ambaye ni mtoto wa mshitakiwa wa kwanza. Ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Wakili Martin Maka...