Rais Magufuli Azua Taaruki Jijini Leo..Aenda Bank ya CRDB na Gari Binafsi Bila Msafara...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezua taharuki mjini leo baada ya kufika katika Tawi la CRDB (Holland Branch), akiwa kwenye gari binafsi lenye namba T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya adamu na hawa wala bendera. Tukio hilo lililochukuwa takribani dakika 25, limetokea majira ya saa nne asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam katika tawi la benki hiyo ambalo liko katika makutano ya Barabara ya Ohio na Samora bila kutarajiwa. Mara baada ya Rais Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo makutano ya barabara hizo yalifungwa huku ndipo rais aliposhuka kwenye gari na kuingia ndani ya benki hiyo. Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliokuwa wakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyo wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao walikwisha ingia. Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kui...