Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MIKATABA YOTE YA JESHI LA POLISI YATAKIWA WIZARANI

MOTO WA RAIS MAGUFULI WAZIDI KUWAKA,MIKATABA YOTE YA JESHI LA POLISI YATAKIWA WIZARANI

Picha
BAADA ya Rais John Magufuli kuizungumzia mikataba ya ujenzi ya Jeshi la Polisi iliyoingia na wawekezaji, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ameitisha mikataba yote ya jeshi hilo. Jeshi la Polisi nchini limetakiwa kuwasilisha mikataba ya miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi askari eneo la Kunduchi, Mikocheni pamoja na Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam pamoja na ule wa majengo mbalimbali ya mwekezaji ambaye Jeshi la Polisi limeingia mkataba naye. Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ikiwa ni miezi miwili tu tangu Rais Magufuli kuzungumzia mikataba hiyo na kuitilia shaka wakati akifungua kikao kazi cha makamanda wa Polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi mjini Dodoma. Meja Jenerali Rwegasira alisema mradi huo ni mkubwa na wa muda mrefu na hivyo ameliagiza jeshi hilo kuuwasilisha mkataba huo, ambao utekelezaji wake unaendelea ili...