BREAKIN NEWZZ!!:- MADAKTARI WA TANZANIA NA INDIA WAFANIKIWA KUFANYA MAAJABU LIVE!!
Gabriel Mwang'onda Madaktari wa Tanzania katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, wakishirikiana na wenzao wa India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa moyo wa aina yake Tanzania. Upasuaji huo ujulikanao kama ‘bypass surgery’ ulishirikisha kupandikizwa kwa mishipa ya damu kutoka sehemu nyingine ya mwili moyoni bila kutumia mashine ya kusimamisha moyo na mapafu. Kwa kawaida madaktari wanasema upasuaji wa moyo hufanyika baada ya moyo na mapafu kusimama, lakini upasuaji huo ulifanyika wakati moyo na mapafu vikifanya kazi. Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa Bashir Nyangasa ameambia BBC kuwa upasuaji huo wa kupandikiza mishipa ya damu nje ya mshine ni wa kihistoria nchini Tanzania. “Mgonjwa anaweza kutolewa mishipa ya damu kutoka miguuni au mikononi baada ya kupewa dawa ya usingizi na mishipa hiyo kupandikizwa kwenye mshipa wa moyo uliokuwa umeziba ili kuruhusu mzunguko wa damu wa moyo kama kawaida bila kutumia mash...