Mshahara wa Rais Magufuli Watua Bungeni.......Mbunge wa Chadema Ataka Upunguzwe na Akatwe Kodi
Suala la mshahara wa Rais, limeibuka tena bungeni ambapo Bunge limeelezwa kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais hawezi kujipunguzia mshahara pindi anapoapishwa kushika wadhifa huo. Hayo yalisemwa bungeni mjini Dodoma jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene, kupitia taarifa aliyoitoa kwa Bunge baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema) kumuomba Rais John Magufuli kujipunguzia mshahara. Mbunge huyo aliyasema hayo wakati akijadili Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2016/17 hadi 2021, ambapo pamoja na kusifu jitihada za Rais Magufuli kwa kuonesha dhamira ya wazi ya kuwajali wananchi masikini na kudhibiti matumizi ya serikali, alimuomba kupunguza mshahara wake na pia kuruhusu ukatwe kodi. “Kwa kweli kwa dhati kabisa nampongeza sana Rais Magufuli kwa namna anavyoonesha wazi kwamba ana dhamira ya kuwatumikia Watanzania. Kwa namna anavyokwenda ni wazi kwamba Rais Magufuli anakuwa ...