Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Sugu Asema Tanzania iliingia Kwenye Soko la Albamu za Muziki Kabla ya Muda Wake

Sugu Asema Tanzania iliingia Kwenye Soko la Albamu za Muziki Kabla ya Muda Wake

Picha
Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema wasanii wa Tanzania waliingia mapema kwenye soko la albamu kabla ya muda wake.  Sugu  Rapa huyo ambaye aliachia wimbo ‘Freedom’ ambao unafanya vizuri kwa sasa, ameiambia Bongo5 kuwa wakati ndio umesabisha soko la albamu kupotea.  “Sisi Tanzania nafikiri tuliwahi kuingia kwenye biashara ya albamu, wenzetu Jamaica wasanii wakubwa kwao, yaani nyumbani kwao Jamaica hawauzi hata nakala elfu 10000, labda wawe International ndio wanaweza kuuza zaidi kazi. Lakini kule kwao ndani waliwekeza kwenye show zaidi na matamasha. Sisi tulianza na albamu bila kuboresha matamasha, na watu wakatuacha huko huko tunagombana na Waindi, na huku show kwa sababu hatukutolea macho wakawa wanatulipa pesa ndogo, kwa sababu tulikuwa hatujui show zina pesa nyingi. Kwa hiyo kilichotokea ni kama mabadiliko, tulianza na ambako pengine hatukutakiwa tuanze, na sasa hivi nyakati ime...