Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Maalim Seif Aruhusiwa Kutoka Hospitali.....Asema Afya Yake Kwa Sasa Imeimarika

Maalim Seif Aruhusiwa Kutoka Hospitali.....Asema Afya Yake Kwa Sasa Imeimarika

Picha
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad aliyelazwa juzi katika Hospitali ya Hindul Mandal aliruhusiwa jana akisema amepona na anaweza hata kushiriki mashindano ya mbio hadi Kibaha.  Maalim Seif juzi alilazwa katika hospitali hiyo baada ya kuugua ghafla akiwa kwenye ndege akitokea Zanzibar kuja Dar es Salaam na aliondoka hospitalini hapo jana saa 12.30 jioni. Akizungumza wa waandishi wa habari, makamu huyo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar alisema madaktari wa hospitali hiyo wamemhudumia vizuri na alianza kupata nafuu baada ya saa tatu, tangu alipofikishwa hospitalini hapo   “Kama mnavyoniona niko ‘fit’, nimelala usingizi mzuri leo na hali yangu imerudi kama kawaida, naweza hata kufanya mashindano ya kukimbia,” alisema baada ya kuteremka kutoka ghorofa ya tatu alikolazwa hadi chini kwa lengo la kuwaeleza waandishi wa habari kuhusu afya yake.  Maalim Seif ambaye alikuwa akitembea kwa ukakamavu, alisema amejisikia faraja baada ya watu wengi kut...