Rais Magufuli Ampaisha Dr. Ramadhani Dau wa NSSF.....Ammwagia Sifa kwa Kazi Nzuri, Azima Ndoto za Wabaya wake
"Kabla sijaanza kuhutubia, naomba nimkaribishe mtu muhimu sana aliyefanikisha ujenzi wa Daraja hili. Dkt Dau tafadhali karibu usalimie kidogo’ ’. Ndivyo alivyoanza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli jana wakati wa uzinduzi wa daraja la kihistoria la kigamboni alilopendekeza liitwe daraja la Nyerere kutukuza mchango wa mwasisi wa taifa hili baba wa taifa hayati mwalimu Julius kambarage nyerere. "Watanzania wana tabia ya kusahau sana. Tunaweza kuzindua hapa wakashangilia lakini wasiwapongeze watu waliofanikisha kazi hiyo..mnyonge mnyongeni haki yake mpeni”. Aliendelea Rais Magufuli mara baada ya Dk. Dau kumaliza kusalimia. Dk Magufuli alisema Balozi Dau alimfuata ofisini kwake(wakati huo akiwa Waziri wa Ujenzi), akiwa mnyonge na mwenye kukata tamaa ya kufanikisha mradi huo. “Ndiyo nikamwambia aanze kufanya kazi.” Rais Magufuli alisema ni Dk Dau na NSSF ndiyo waliosimamia na kuhakikisha d...