Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mkurugenzi Maswa Afariki Dunia Ghafla Kabla ya Ziara ya Waziri Mkuu

Mkurugenzi Maswa Afariki Dunia Ghafla Kabla ya Ziara ya Waziri Mkuu

Picha
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekatisha ziara yake ya siku sita mkoani Simiyu, baada ya kifo cha ghafla  cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa (DED), Trasias Kagenzi kilichotokea juzi usiku. Kaimu Katibu Tawala, Donatus Weginah alithibitisha kutokea kifo cha mkurugenzi huyo wakati Waziri Mkuu akiwa na ratiba ya kutembelea wilaya hiyo. Weginah alisema juzi asubuhi Kagenzi alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia akiwa na mlinzi wake na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Rosemary Kirigini lakini alianza kujisikia vibaya. “Mkurugenzi alikuwa akifanya mazoezi ‘jogging’ na DC Rosemary Kirigini, lakini baadaye alimwambia Kirigini najisikia pumzi zinabana, akamwambia aendelee… lakini mara mkuu wa wilaya alimuona amejiinamia, aliporudi kumuuliza akamwambia naona nakosa hewa, ndipo alipoamua kukimbia kuchukua gari kumpeleka hospitalini,”alisema. Weginah alisema mkurugenzi huyo alipelekwa hospitali na majira ya saa tano asubuhi alionekana akiendelea vizuri, ha...