Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TATOA WAMPONGEZA JPM KWA BOMBA LA MAFUTA ...

TATOA WAMPONGEZA JPM KWA BOMBA LA MAFUTA ...!!!

Picha
WASAFIRISHAJI nchini wamempongeza Raisi John Magufuli kwa juhudi zake zilizoiwezesha Tanzania kupata mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta litakalojengwa kutoka Uganda hadi Tanga. Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) pia kimeipongeza timu ya mazungumzo iliyoongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, huku kikiwataka wanachama wake na wadau wote kwa ujumla kuchangamkia fursa nyingi na kubwa za kibiashara zitakazotokana na ujenzi wa bomba hilo. “Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa rais wetu na timu iliyoshiriki kwenye mazungumzo, wametufanyia jambo kubwa katika ujenzi wa uchumi wa nchi...imebaki juu yetu kupanga mikakati ya namna ya kutumia fursa za kibiashara zitakazoletwa na mradi huu,” alisema Mwenyekiti wa Tatoa, Angelina Ngalula jijini Dar es Salaam jana. Ngalula alisema kutokana na fursa hii kubwa iliyopatikana, wadau wote wa bandari wana wajibu wa kuitumia katika kutangaza bandari zilizopo nchini ili kuvutia wawekezaji na wateja ka...