Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kopa

Kopa, Msaga Sumu kupagawisha ‘Amsha Mama’ kesho

Picha
Mkali wa miondoko ya Mipasho, Khadija Kopa (kushoto), akiongea na kujigamba jinsi alivyodhamiria kufanya makamuzi ya kufa mtu kwenye tamasha la Amsha Mama Festival katika viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam kesho. Kulia ni Mratibu Mkuu wa tamsha hilo, Joe Kariuki, akimsikiliza kwa makini msanii huyo kwenye kikao cha waandishi wa habari kilichofanyika ndani ya Hoteli ya Travertine Magomeni jijini Dar es Salaama MKONGWE wa miondoko ya mipasho nchini, Khadija Kopa, na mkali wa Singeli, Msaga Sumu, hatimaye wamejitokeza na kujigamba kuwa kesho wataonyesha maajabu ya nguvu katika tamasha la Amsha Mama Festival litakalofanyika katika Viwanja vya Mwembe-Yanga Temeke jijini Dar es Salaam. Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar, Khadija Kopa na Msaga Sumu walisema kwamba kwa makamuzi waliyojipanga nayo kesho kwenye tamasha hilo kuna hatari ya ‘kufia jukwaani’ kwani wamejipanga kutoa burudani kwa wakazi wa Teme...