Jerry Muro:Pesa za CAF Tutaisaidia Simba Kulipa Deni la Musoti Wasije Shushwa Daraja
Klabu ya Yanga kupitia kwa mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Jerry Muro, wamesema wako tayari kuisaidia Simba kulipa deni la Musoti ili klabu hiyo ya Msimbazi isishushwe daraja. Muro amsema, wako tayari kuichangia Simba kulipa deni lao linalowakabili ili FIFA isiishushe daraja na wao wakakosa pointi sita katika msimu ujao wa VPL. “Tunaomba watuletee barua na karatasi za malipo za yule mchezaji ili sisi tu-process malipo kwa sababu tuliahidi tukifika hatua ya makundi ya michuano ya Afrika tutawasaidia kulipa deni lao. Sisi hatukubali Simba ishushwe daraja kwasababu pale tunapointi sita za wazi kwenye msimu ujao wa ligi”. “Sasa kwanini tukose pointi sita ambazo tunaweza tukazitetea zikabaki. Inaweza ikashuka Simba halafu ikapanda timu ya Milambo ya Tabora halafu ikatusumbua sana, sisi tunazihitaji ponti sita za Simba na tulisema tukifika hatua ya makundin tutawalipia”. “Ili tuweze kufanya transaction na kwakua hela hii in...