KAMA UMESHINDWA KABISA KUTOA KITAMBI NA KUPUNGUA UZITO KABISA SULUHISHO HILI HAPA
Huenda wewe msomaji umeshakata tama kabisa ya kupungua uzito baada ya kutumia njia mbalimbali bila mafanikio, lakini naomba nikupe matumaini kwamba swala la kupunguza uzito na kutoa kitambi linawezekana kabisa na sio gumu kama watu wanavyofikiria. Leo ntaenda kutoa elimu muhimu sana ambayo ukiifuata kwa makini utapungua uzito. Pamoja na kua daktari, miaka ya nyuma nilikua mnene sana hivyo naongea mambo ambayo nimeyapitia.Kiukweli unene unatesa sana kimwili na kisaikolojia, yaani uchovu mara kwa mara, jamii inakuona tofauti sana na huenda hata kupata mpenzi ikawa ngumu kidogo, kukosa baadhi ya kazi na kushindwa hata kuvaa baadhi ya nguo kwa ajili ya unene lakini hebu tuyaache hayo tuongelee maada kuu.Formula ya unene ni ndogo sana, ukila sana kuliko shughuli au mazoezi unayofanya unaongezeka uzito, ukila kidogo na kufanya mazoezi sana unapungua uzito, kiasi unachokula kikilingana na shughuli na mazoezi unayofanya unabaki kwenye uzito ule ule. Lakini kupunguza uzito inatakiwa mtu u...