Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Ester Bulaya Achafua Hali ya Hewa Bungeni Baada ya Kumfananisha Waziri Maghembe na TISHU

Ester Bulaya Achafua Hali ya Hewa Bungeni Baada ya Kumfananisha Waziri Maghembe na TISHU

Picha
Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya jana alichafua hali ya hewa bungeni baada ya kusema kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ni mzigo na mwepesi kama ‘tishu’ kwa sababu hana uwezo wa kusimamia mambo mazito yaliyopo katika wizara hiyo, kama vile migogoro ya wananchi na hifadhi za Taifa. “Huyu waziri ni mzigo kama alivyowahi kusema (Abdulrahman) Kinana. Mimi nasema yeye ni mwepesi kama tishu, hawezi kuisaidia wizara hii nyeti,” alisema mbunge huyo jana wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama alisimama na kuomba mwongozo wa mwenyekiti juu ya mbunge huyo kutumia maneno ya kuudhi ambao uliungwa mkono na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliyemtaka Bulaya kufuta neno mwepesi kisha aendelee na hotuba yake. Hata hivyo, Bulaya alikataa kufuta neno hilo na kusema wabunge hawaamuliwi maneno ya kutumia. Chenge aliendelea kumsihi mbunge huyo kufuta ...