Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Rais wa Vietnam Kutua Nchini Kesho Saa Mbili Usiku

Rais wa Vietnam Kutua Nchini Kesho Saa Mbili Usiku

Picha
RAIS wa Vietnam, Truong Tan Sang anatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara rasmi ya kiserikali akifuatana na mke wake Mai Thi, mawaziri watano na wafanyabiashara 51.  Hii ni ziara ya kwanza ya Mkuu wa nchi kuzuru nchini tangu Rais John Magufuli aingie Ikulu, lakini pia itakuwa ziara ya kwanza kwa Rais Truong kuzuru Afrika na Tanzania na baadaye ataelekea Msumbiji. Pamoja na kuwa na mazungumzo na Rais Magufuli, Rais Truong atakutana na Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, Spika wa Bunge Job Ndugai na kushiriki dhifa ya kitaifa Ikulu.  Atakapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam saa 2.30 usiku kesho, Rais Truong atapokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk Augustine Mahiga. Mapokezi rasmi kwa Rais huyo yatafanyika Jumatano Ikulu, Dar es Salaam ambapo kama zilivyo taratibu za kidiplomasia duniani, atapigiwa mizinga 21 na kukag...