RAIS MAGUFULI AONGOZWA KUPIGWA JUJU,VIGOGO WAHAHA KILA KUKICHA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ Mwandishi wetu, Amani DAR ES SALAAM: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’, huenda ndiye mtu anayeongoza kwa kupigwa juju kwa waganga wa kienyeji kuliko mtu yeyote nchini kwa sasa, Amani linakuja na ushuhuda. Sangoma mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shark Abdullah ‘Kishapu’, akipiga simu kutoka jijini Tanga mwanzoni mwa wiki hii, aliliambia gazeti hili kuwa katika miezi ya hivi karibuni, amekuwa akipata wateja, wakiwemo wafanyabiashara na watumishi wa umma wakimtaka kumpunguza kasi ya utendaji kiongozi huyo, wakisema inawaathiri. “Sikiliza ndugu mwandishi, mimi hapa ni mganga wa kienyeji, nataka nikupe habari. Kuna watu wengi sana wanakuja hapa kwangu kutaka niwakinge na tumbuatumbua ya Magufuli, wengine wanataka nifanye ninavyoweza kumfanya asiweze kutekeleza majukumu yake. “Nimewapokea wafanyabiashara na hata vio...