PICHA:Makamu Wa Rais Mhe. Samia Azindua Mbio Za Mwenge Wa Uhuru Mkoani Morogoro Leo
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro leo. Katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais alimnukuu Baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere akisema kuwa nia ya Mwenge wa Uhuru tangu mwanzo ni kumulika mipaka ya nchi yetu dhidi ya maadui, kuleta matumaini pale ambapo hakuna matumaini, kuondoa chuki pale ambapo kuna chuki na kuleta heshima pale ambapo kuna dharau. Alisema nia hiyo ya kuwepo kwa Mwenge wa Uhuru kama alivyomnukuu Baba wa Taifa, inaendana na dhana ya kutumbua majipu katika Serikali ya awamu ya tano. Alisema utumbuaji majipu unalenga kuleta matumaini kwa wananchi ambao wamekata tamaa na kuleta heshima kwa wananchi waliodharauliwa. “Kaulimbiu ya mbio ya za mwenge mwaka huu ni hii: Vijana ni nguvu kazi ya taifa, washirikishwe na wawezeshwe,”alisema Makamu wa Rais na kuongeza kuwa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa hawajatumika ipasavyo kutokana na sababu mbalimbali. Alizit...