Waafrika wataka uwekezaji zaidi katika sekta ya maji
Viongozi wa nchi za Kiafrika wametoa wito wa kuwekeza zaidi katika sekta ya maji ili kurahisisha upatikanaji wa maji barani humo.Nchi zilizoshiriki katika mkutano wa kimataifa wa 18 wa Jumuiya ya Maji Barani Afrika (African Water Association) AFWA kwa kifupi, zilikamilisha mkutano wao jana mjini Nairobi kwa kusisitiza udharura wa kuvutia vitega uchumi zaidi kwa ajili ya kusafisha maji na kuwawezesha watu kupata vyanzo vya maji masafi.Taarifa iliyotolewa na viongozi wa Afrika walioshiriki mkutano huo imesema kuwa, kuna udharura wa kupewa kipaumbele stratijia mpya ya kusaidia kupatikana utatuzi wa mgogoro wa maji katika maeneo ya mijini na vijijini barani Afrika.William Ruto ambaye aliwakilisha Kenya katiuka mkutano huo amezitaka nchi za Afrika kutumia njia mpya kwa ajili ya kutimiza malengo ya ustawi endelevu hususan kutayarisha maji safi.Karibu wawakilishi wa nchi nyingi za Afrika wameshirika katika mkutano huo ulioanza kazi zake Jumatatu iliyopita kwa hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta wa...