Lady Jaydee Kutoa Kauli yake Leo Baada ya Kudai Kudhalilishwa na Gardner
Siku 14 tangu Mtangazaji wa Clouds Fm Gardner Habash kudaiwa kutoa lugha ya udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mke wake Judith Wambura, mwanamuziki huyo maarufu kwa jina la Lady Jaydee, amesema leo anatarajia kutoa tamko rasmi kuhusu suala hilo. Buff Bantam Hen {Gallus gallus domesticus} with nine of her ten chicks, 2-days-old. The tenth chick is under her “Nipo katika maandalizi ya tamasha langu ndiyo maana ilikuwa vigumu kwangu kulizungumzia hili, Jumatatu (leo) nitatoa tamko,” alisema Jaydee. Mei 13 kupitia mwanasheria wake Amani Tenga kutoka kampuni ya Law Associates Advocate, alimwandikia barua ya kumtaka mtangazaji wa Clouds Fm, Gardner Habash kuomba radhi mbele ya umma ndani ya siku 7 kwa kauli ya udhalilishaji aliyoitoa dhidi yake. Gardner anadaiwa kutamka maneno ya udhalilishaji dhidi ya Jaydee Mei 6 mwaka huu na kurekodiwa kisha video kusambazwa katika mitandao ya kijamii, katika ukumbi wa CDS PARK (zamani TCC) alipokuwa akisherehesha tamasha la Miss TIA 2016, ...