JE WAJUA UKWELI KUHUSU BANGI?
Bangi ni neno ambalo hutumika kuelelezea sehemu iliyokaushwa ya maua, mbegu, mche na majani ya mmea ujulikanao kama Indian hemp. Uko mitaani bangi ina majina mengi na watumiaji wake wameipa majina kama: dope, nyasi, majani, mche, ganja, magugu, kitu, sigara kali, blanti na mboga. Kwa kitaalam “cannabis” huelezea aina mbali mbali za dawa za kulevya zitokanazo na mmea wa Indian hemp ambazo ni bangi (marijuana) na hashish. Aina hizi za dawa zitokanazo na mmea huu ziko katika kundi la dawa za kulevya ziletazo maruweruwe (hallucinogen) au dawa zinazoathiri ubongo na kubadili jinsi tunavyotazama mambo katika uhalisia wake.Kuna zaidi ya aina 400 za kemikali katika mmea huu na kemikali ya kulaumiwa inayohusika na mabadiliko haya katika ubongo hujulikana kama tetrahydrocannabinol (THC). Kiasi cha THC hutofautiana kulingana na eneo ulikolimwa mmea wa Indian hemp. Kama tulivyoona bangi ni sehemu iliyokaushwa ya majani, mbegu,maua, na mche na huwa na rangi ya kijani,kijivu au brau...