Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Ali Kiba Alikuwa Analia Studio -Chid Benz

Ali Kiba Alikuwa Analia Studio -Chid Benz

Picha
Msanii Chid Benz alimaarufu kama Chuma amefunguka na kusema wakati wana rekodi wimbo wa ‘Hasira za Nini’ ambao alimshirikisha Ali Kiba. Anadai ilifika mahali msanii King Kiba alidondosha chozi. Kupitia kipindi Cha Planet Bongo cha East Africa Radio ambapo Chid benz alipewa “Heshima ya bongo fleva” alifunguka na kusema wakati wapo Mj Records kufanya kazi hiyo Ali Kiba alidondosha chozi sababu yeye alimfungia mlango ndani na kumwambia hawezi kutoka mpaka atakapo maliza kuweka vocal. “Unajua mdogo wangu Ali Kiba alipoingia booth mimi nikamfungia mlango kabisa ili asitoke so akawa analalamika maana mle ndani kulikuwa na joto sana, lakini nikamwambia mdogo wangu huwezi kutoka mpaka umalize kazi baada ya hapo akalia kisha akakaa zake chini baadae aliinuka na kuendelea na kazi mpaka mzigo ulipoisha ndio nikamfungulia mlango na kutoka ” Amesema Chid Benz Katika hatua nyingine Chid Benz amesema licha ya yeye kufanya muziki wa Hip hop lakini alikuwa na mash...