TanzaniteOne Yamvaa Mbunge James Ole Millya, Yamtuhumu Kupotosha Bunge na Umma Bila Kufanya Utafiti
Lema Akiwa na James ole MillyaKAMPUNI ya Sky Group Associates inayomiliki mgodi wa tanzanite wa TanzaniteOne, imesema Mbunge wa Simanjiro, James ole Millya amepotosha Bunge na umma juu ya suala zima la ununuzi wa hisa kwa kampuni hiyo. Akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini mwishoni mwa wiki, Millya alisema Sky Group Associates iliyonunua hisa kwa Kampuni ya TanzaniteOne na kumiliki kitalu C Mirerani wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, haikufuata taratibu za ununuzi wa hisa hizo na kuwatuhumu baadhi ya mawaziri kuwa walihusika katika kupindisha taratibu. Aliwataja mawaziri hao kuwa ni George Simbachawene na Jenista Mhagama, ambaye hata hivyo alikanusha madai hayo ; na ametaka taratibu za Kibunge zimlamzishe Millya, kukanusha au kuthibitisha madai yake. Mbali ya hilo, mbunge huyo aliituhumu kampuni hiyo kwa kuwafukuza kazi wafanyakazi 201, bila ya kufuata utaratibu na kwamba inawanyanyasa . Akizungumza na mwandishi wetu, Mwanasheria wa ka...