Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Uingereza Kusaidia Usambazaji wa Umeme Vijijini

Uingereza Kusaidia Usambazaji wa Umeme Vijijini

Picha
Miezi  michache baada ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) kujitoa kusaidia Tanzania katika usambazaji wa umeme vijijini, Serikali ya Uingereza kupitia taasisi yake ya Energy Africa Initiative, imetangaza utayari wa kutoa msaada huo. Waziri wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa, Justine Greening, ameeleza utayari huo mwishoni mwa wiki, katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliye nchini humo kumwakilisha Rais John Magufuli, katika mkutano wa kimataifa wa kupambana na rushwa duniani. Katika mazungumzo hayo, Greening alimhakikishia Waziri Mkuu Majaliwa, kwamba nchi yake iko tayari kuisaidia Tanzania kwenye mpango wake wa kupeleka umeme vijijini. “Tuko tayari kuwasaidia kutekeleza mpango huu kupitia taasisi ya Energy Africa Initiative ambayo inapata ufadhili kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID),”  alisema.  Pia Waziri huyo wa Uingereza, alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya T...