Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya ULAJI BORA KWA AFYA

ULAJI BORA KWA AFYA

Picha
Ulaji bora kiafya siyo suala la masharti magumu katika filosofia ya lishe bora,pia siyo kuwa mwembamba sana au kujinyima vyakula unavyopenda. Isipokuwa ni kula vyakula vitakavyokufanya ujisikie vizuri, kukuongezea nguvu mwilini, kuweka sawa afya ya akili na kujiweka katika hali nzuri ya afya kwa kadiri iwezekanavyo; yote yanawezekana kwa kujifunza baadhi ya kanuni za msingi za lishe bora kwa jinsi itakavyokuwa bora kwako. Watu wengi hufikiri kuwa lishe bora ni kula kwa wingi na siyo suala la  kuzingatia  mlo kamili, lakini msingi mkuu ni kula kwa kiasi chakula bora. Kiasi ni nini? Kiasi ni kiwango gani? Tunaposema kiasi, hiyo inategemea na mtu mwenyewe na tabia aliyojijengea katika ulaji wa chakula. Lengo la  ulaji wa chakula bora kwa afya bora ni kujenga tabia ya kula aina ya lishe bora ambayo utaendelea kula kwa maisha yako yote, siyo tu kwa wiki chache au miezi michache mpaka pale utakapokuwa umefikia uzito ulio sawa kwa afya. Kwa hiyo jaribu kufikiri kiasi ambacho k...