Mwenyekiti Wa Mtaa Wa Babale Uliopo Wilaya Ya Nyamagana Jijini Mwanza Auawa Kwa Kupigwa Risasi Na Watu Wasiofahamika
MWENYEKITI wa Mtaa wa Bulale wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Alphonce Nyinzi (48) ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika wakati akielekea nyumbani kwake. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Ahmed Msangi amesema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 22 mwaka huu majira ya saa 2 usiku. Msangi amesema kuwa marehemu aliekuwa akifahamika kwa jina maarufu "msukuma" mfanyabiashara na mkazi wa bulale aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani na kutokea chini ya kwapa upande wa kulia na watu wawili wasio fahamika pamoja na risasi hiyo kumjeruhi Neema Marangula (23) Mkazi wa Bulale katika Kiganja cha mkono wa kulia. Amesema kuwa wakati Mwenyekiti huyo akitoka kwenye kikao alichofanya na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtaa wa Bulale akiongozana na wajumbe wawili alikutana na Neema Marangula akiwa na mume wake ambao walikua wanawafuata marehemu na Balozi kwa ajili ya kuzungumzia mzozo wa ndani ya...