Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya sisaini Yanga

Yondani: Bila mil 60, sisaini Yanga

Picha
Dar es Salaam BEKI wa kati tegemeo wa Yanga, Kelvin Yondani, anataka kubaki kuendelea kukipiga na timu hiyo lakini amesisitiza anataka awekewe mezani kitita cha Sh milioni 60 ili asaini mkataba mpya. Yondani hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kutokana na kubakiza miezi miwili tu kwenye mkataba wake. Beki huyo ambaye ni kipenzi cha Mholanzi, Hans van Der Pluijm, alijiunga na Yanga msimu wa 2011/2012 akitokea Simba baada ya mkataba wake kumalizika. Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Kamati ya Utendaji ya Yanga, beki huyo yupo kwenye mazungumzo na timu hiyo na tayari amewatajia dau la fedha analolihitaji ambalo ni shilingi milioni 60 ili aendelee kubaki kwenye timu hiyo. Chanzo hicho kilisema beki huyo ameonyesha nia kubwa ya kubaki kuendelea kuichezea Yanga msimu ujao, lakini kama atapewa fedha hizo anazozihitaji. Tofauti na dau hilo, pia beki huyo ameomba aboresh...