Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Wapinzani Walegeza......Waahidi Kuwasilisha Vipande Muhimu vya Hotuba Kivuli ya Bajeti

Wapinzani Walegeza......Waahidi Kuwasilisha Vipande Muhimu vya Hotuba Kivuli ya Bajeti

Picha
Wakati hatua ya upinzani kumsusia Naibu Spika, Dk Tulia Ackson ikiingia siku ya nane, Kambi ya upinzani imesema leo itawasilisha vipande muhimu vya hotuba kivuli ya bajeti ambavyo ni vya msingi. Naibu msemaji wa kambi hiyo kwa Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde alisema kutokana na umuhimu wa vipande hivyo ambavyo hakuvitaja, atavisoma kwa ufupi na kuviwasilisha, kisha kuondoka. Wabunge wa upinzani walianza kususia vikao anavyoongoza Dk Tulia Jumanne ya wiki iliyopita, kufuatia kitendo cha kiongozi huyo kuzuia hoja ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kuhusu kutimuliwa kwa wanafunzi 7,802 wa chuo kikuu cha Dodoma (Udom). Jumatatu ya wiki iliyopita Dk Tulia alizuia hoja ya Nassari akieleza kuwa kutokana na anavyoona sakata hilo la wanafunzi wa Udom halikuwa la muhimu kusimamisha shughuli za Bunge kwa wakati huo kwa kuwa Serikali tayari ilishatoa majibu. Kitendo hicho kilisababisha wabunge wa upinzani kupinga uamuzi huo jambo lililosababisha Dk Tulia kuahirisha shug...