LHRC Yaonya Kuhusu Picha za Uchi na za Kutisha
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeonya vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu kuchapisha picha za utupu ama za kutisha katika mitandao ya kijamii. Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam , Mkurungenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dk. Helen Kijo Bisimbaalisema kuwa, kumekuwa na matukio kadha yanayofanywa na watu juu ya kurekodi na kupiga picha ambazo sio nzuri kwa mujibu wa sheria. Alibainisha picha hizo kuwa ni pamoja na matukio ya mauaji, ajali za kutisha na miili ya marehemu zinazochapichwa katika mutandao ya kijamii, blog na hata baadhi ya vyombo vya habari bila kijali kwamba, kufanya hivyo ni kinyume cha sheria. Dk. Kijo alisema kuwa, tarehe 4 Mei mwaka huu katika Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo picha za miili ya marehemu (mama na mtoto) ambayo majina yao yamehifaziwa, zilisambazwa katika mitandao ya kijamii zikionesha majeraha ya kutisha kutokana na kitendo cha kinyama kilichofanywa. Katika tukio...