Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kinachosababisha macho kutoona

Kinachosababisha macho kutoona

Picha
Macho ni moja ya milango mitano ya fahamu. Kazi yake ni kuhakikisha binadamu anaona mazingira yanayomzunguka. Bila macho huwa ni vigumu kwa binadamu kuyatawala mazingira yake. Ili kuweza kutawala vyema mazingira yake binadamu anahitaji macho ambayo yanaona vizuri na mfumo wa fahamu ambao unaweza kutafsiri mwanga wa taswira ambao unafikishwa kwenye ubongo kupitia macho. Kwenye makala yetu leo hii tunaangalia changamoto mbalimbali ambazo zinasababisha macho kushindwa kuona vizuri na matokeo yake kusababisha taswira yenye kasoro kwa ajili ya kutafsiriwa na ubongo. Macho kushindwa kuona vizuri husababisha mwanga wa taswira unaopelekwa kwenye ubongo kupitia mshipa maalumu wa fahamu wa macho kuwa na upungufu. Ingawa tatizo linaweza kuwa kwenye jicho moja mara nyingi madhara yake kwenye tafsiri inayofanywa na ubongo huhusisha macho yote. Dalili ni kama vile kuona taswira mbili tofauti kutokana na jicho moja kuona vizuri na jingine kutoona vizuri, kushindwa kuona au kupata matatizo ya kuo...