Tume ya uchaguzi DRC yataka muda zaidi kujitayarisha kwa ajili ya uchaguzi
Tume Huru ya Uchaguzi Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENI) imeomba muda zaidi wa kujitayarisha kwa ajili ya kuandaa zoezi la uchaguzi wa rais. Mkuu wa CENI Corneille Nangaa amesema anahitaji takribani miezi 16 ili kuandaa kwa njia sahihi uchaguzi ujao wa rais nchini humo. Akizungumza mjini Kinshasa, Nangaa amesema tume hiyo inapaswa kuandikisha wapiga kura na kutayarisha daftari jipya la wapiga kura na kwamba zoezi hilo linahitaji miezi 16. Aidha mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi DRC amesema tume hiyo imewasilisha ombi hilo kwa Umoja wa Mataifa na kwamba azimio 2277 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilihusu ombi hilo. Azimio hilo lilitaka serikali ya DRC iandae uchaguzi wa rais kwa mujibu wa katiba ya nchi. Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anakamilisha duru yake ya urais tarehe 19 Desemba mwaka 2016. Pamoja na hayo tume ya uchaguzi nchini humo inasema inahitajia zaidi ya dola bilioni moja ili kuandaa uchaguzi wa rais kwa mafanikio. Tangazo hilo...