China Wammwagia Sifa Rais Magufuli....Wasema Kaipaisha Tanzania Kimataifa
SERIKALI ya China imeiunga mkono serikali katika mkakati wake wa kutoa elimu bure, ikisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, Tanzania inasifika duniani. Katika kuunga mkono elimu bure, ubalozi wa nchi hiyo nchini umetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 28 kwa shule mbalimbali za msingi katika wilaya ya Iramba mkoani Singida. Balozi wa China hapa nchini, Dk Lu Youq’ng alisema msaada huo ni moja ya juhudi za nchi yake kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kutoa elimu bure. “Wakati mimi nimechangia madawati 300, Kampuni inayochimba madini hapa ya Sun Shine Group imechangia madawati 100 ili kuniunga mkono,” alifafanua. Akikabidhi madawati hayo katika mikutano mitatu tofauti kwenye mji wa Kiomboi, Shelui na Misigiri, Balozi Youq’ng alisisitiza umuhimu wa Tanzania kuwekeza kwenye elimu kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kweli. “Hata kama nchi ni maskini kiasi gani, lazima elimu itiliwe mkazo; tena...