Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Waendelea Kupungua.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2016 na kusema kuwa umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.4 iliyokuwepo mwezi Machi, 2016. Hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa mwezi Aprili 2016 imepungua kidogo ikilinganishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma iliyokuwepo mwezi Machi mwaka huu. Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo ametoa taarifa hiyo jana jijini Dar es salaam na kueleza kuwa kupungua kwa mfumuko huo kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali nchini. Alisema Takwimu zilizokusanywa katika mikoa yote ya Tanzania Bara kwenye bidhaa zinazotumika kupima mfumuko wa bei kwa mwezi Aprili 2016 zimeainisha kuwa bidhaa zisizo za vyakula katika soko zikiwemo Gesi , dizeli na mafuta ya taa zimechangia ku...