Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Aspirini Tumaini jipya kwa wagonjwa wa saratani

Aspirini Tumaini jipya kwa wagonjwa wa saratani

Picha
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza, wengi tumekuwa tukiichukulia dawa ya aspirini kama dawa ya hadhi ya chini, hatufahamu kuwa ina uwezo mkubwa wa kitiba mwilini ikiwamo kuzuia magonjwa ya moyo na kiharusi. Mamilioni ya watu duniani humeza vidonge hivyo kupunguza hatari ya kufa kwa magonjwa ya moyo na kiharusi baada ya kupewa ushauri na wataalamu wa afya. Tafiti mpya zinaleta tumaini jipya kwa wagonjwa wa saratani, matokeo chanya ya tafiti mbalimbali duniani yanaleta ushahidi mpya ya uwezekano wa dawa hii kuzuia na kutibu saratani mbalimbali. Kwa mujibu wa taasisi za dawa za ndani na nje ya nchi, dawa hii ambayo ni moja ya dawa zisizo na gharama ni salama kwa matumizi ya binadamu. Taarifa za kitabibu na kifamasia zinaonyesha kuwa faida ya kutumia dawa hii ni kubwa kuliko madhara machache yanayojitokeza, ndiyo maana haikuwahi kuzuiwa kwa matumizi ya binadamu. Miaka ya nyuma dawa hii ilikuwa mwokozi wa kila siku kwa watu wengi, hasa waliopatwa na maumivu ya mwili na homa. B...